Mtoto wa Lulu Hassan atolewa nje kwa mara ya kwanza.

News

 

By;Elisha Odoyo


Mwanahabari wa Citizen TV Lulu Hassan alijifungua mtoto wa tatu mwezi uliopita lakini tangu kumpata mtoto huyo hajazungumza. Wakenya walizipokea kwa furaha habari hizo na kutamani kumwona mtoto wake lakini baada ya wiki kadhaa, amejitokeza na kuzungumzia suala hilo.


 Mnamo Ijumaa, Okotoba 12, mtoto wa Lulu alitimia siku 40 na aliitumia siku hii kumtoa nje kwa sherehe iliyowaleta wanahabari wa kike marafiki zake kumkaribisha. Miongoni mwa waliofika kwenye sherehe hiyo ni Msemaji wa Ikulu Kanze Dena, na wafanyakazi katika tasnia ya uanahabari kama vile Ann Mawathe, Wilkister Nyabwa, Mercy Kandie walioonekana katika picha ya Instagram aliyoichapisha Lulu,
Lulu na mume wake Rashid walimpata mtoto huyo mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya kuufanya ujauzito huo siri kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *